Wednesday, February 17, 2010

Ukristo Unorwe

Muda wasonga na mawazo yanizidi.
Ni kweli kwamba sote tuna mtazama Yesu Kristo aliye mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Baba (Waebrania 12:2).

Kwa Mkristo aliyetoka nchi za kusini, wacha niseme Kenya, kuwa Mkristo ni uamuzi wa muhimu. Katika nchi za Kaskazini, nafikiri ni virahisi sana kusahau umuhimu wa kumtegemea Mungu... nafikiri pengine ni kwa sababu maisha ni shwari, hakuna matata!...

Jambo hili limenifanya niwaze sana kuhusu tofauti ya Ukristo kusini na kaskazini! Naendelea kuwaza na pia kuwaza pamoja na wanafunzi ninaokutana nao mara si haba!
Tofauti moja kuu ni kuwa Wakristo wengi wamekuwa Wakristo tangu utotoni na kuendelea kuishi maisha ya ukristo. Juzi pia nilikutana na msichana ambaye alikuwa Mkristo akiwa amekomaa na alinieleza anaendelea kuelewa maisha ya Ukristo. Kule Kenya, kukiri kwamba Yesu ni Bwana na kutubu dhambi ndilo jambo linasababisha mtu kuwa Mkristo.

Kuna jambo lingine ambalo niliweza kutambua wiki mbili zilizopita, kwamba kuna Wakristo (very charismatic) pia - nilipoingia katika kanisa hilo, nilidhania niko Kenya! Lakini pia nimefurahi nyakati zile za kuomba ambapo watu wote wamenyamaza ti - nimeona hili ni jambo la muhimu na pia kumpa Mungu heshima!

Mawazo yanazidi na naendelea kuwaza! Natumai Bwana Yesu ataniwezesha kuwaza ndani Yake!

0 comments: